Tuesday 16 November 2010

Njenje usiku wa Idd Muscat









Siku ya Idd Mosi ilikuwa siku yenye kuleta faraja nyingi kwa wanamuziki wa Kilimanjaro Band. Tuliweza kutembelea bendi mbili kati ya tatu zinazotoka Tanzania ambazo ziko hapa Muscat. Jambo lililoleta faraja kubwa ni kukuta bendi hizo zikipiga nyimbo kadhaa za Njenje na tena kwa ufasaha mkubwa. Faraja ilikuwa ni ya aina mbili, kwanza kuwa tungo zetu nyingine za miaka mingi bado zinapendwa, na jingine ni kuwa kuna vijana wa Kitanzania wanaendeleza kwa ufasaha gurudumu letu. Tulijisikia tumepwa heshima kubwa na wanamuziki hawa kwa kuona kuwa kwa kupiga nyimbo zetu waliona kuwa wanapiga kitu kizuri katika show zao. Tulipokelewa vizuri, na kati ya maneno ambayo yalifurahisha ni ya mtoto wa mwanamuziki Hamza Kalala, ambae hujitambulisha kama Totoo Kalala aliyesema, " Wazee endeleeni kutunga ili tuwaige nasi tuweze kula".

2 comments:

  1. Karibuni sana nyumbani wana njenje na poleni kwa safari. Naona leo ni KEMPISKI mnakamua moja kwa moja toka AIR port . Kweli ninyi ni watu wa kazi

    ReplyDelete
  2. Waweja nguruma yashiraga wananjenje.

    ReplyDelete

ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA