ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

Jumatatu, 21 Machi 2011

Wasanii 13 wa Five Stars Modern taarab wafariki katika ajali mbaya


Bi Mwanahawa amenusurika japo kajeruhiwa vibaya
Kundi la Five Stars Modern Taarab limepata ajali mbaya sehemu za Mikumi wakiwa safarini kutokea Songea. Inasemekana ajali hiyo ilitokea baada ya  basi dogo walilokuwemo wasanii hao kugonga roli lililokuwa limeharibika. Wasanii 13 akiwemo mpiga solo Sheba Juma, Nassoro Madenge, Husna Mapande na Issa Kijoti, inasemekana wamefariki wakati wengine ni mahututi na wamekimbizwa Morogoro. Kundi hili lililokuwa linajulikana pia kama 'Watoto wa Bongo' lilizinduliwa Msasani Club tarehe 29 July 2009. Tunaomba  Mungu awalaze pema wote waliofariki na awanusuru waliojeruhiwa. Mwimbaji mashuhuri Bi Mwanahawa aliyeimba wimbo Kinyago cha Mpapure wakati akiwa East African Melody anusurika
Five Stars siku ya uzinduzi wa kundi lao
Wapiga magita wa Five Stars, Musa na Sheba

Wanamuziki wa Five Stars Watoto wa Bongo

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.

KAMA KAWAIDA NJENJE JUKWAANI LEO JUMAMOSI

KAMA KAWAIDA YA KILA JUMAMOSI BENDI YAKO YA KILIMANJARO WANANJENJE ITAKUWA JUKWAANI PALE SALANDER BRIDGE CLUB LEO KUANZIA SAA NNE USIKU NA...