ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

Jumapili, 3 Aprili 2011

Wangu ngaiyeeee ngoma iko huku

Wimbo huu ni utunzi wa marehemu Salum Yazidu Abdallah(SAY), ukifika Morogoro utaona maroli yameandikwa SAY hicho ndio kirefu chake. Huyu alikuwa kiongozi wa Cuban Marimba Band. Na huu ulikuwa mmoja wa nyimbo zao nyingi zilizotikisa anga la Afrika Mashariki katika miaka ya 1963-1965. Hapa zimeunganishwa nyimbo mbili mwingine ukiwa Ee Mola wangu. Huu wa pili ulikuwa ni tenzi ndefu aliyoitunga na kuchukua beti chache na kurekodi, na ulikuwa kama ndio utabiri wa kifo chake. Alifariki mwaka 1965 wakati akiwa katika moja ya roli lake wakati akisafirisha mawe jioni hivi taa za gari zikazimika ghafla na gari ikagonga mgema akatupwa nje na kupasuka kibofu. Angalia utunzi ulivyokuwa mahiri, ni miaka zaidi ya arobaini toka nyimbo hizi zilipotungwa lakini bado zinaleta raha. Mungu amlaze pema peponi Salum Abdallah

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

Hongera sana wana njenje,hivi ndivyo inatakiwa miziki yetu ya Tanzania isikike,yaani ina utambulisho wazi kuonyesha muziki huu ni wa ki Tanazania.Pia mnafanya vizuri sana kuwa na "identity"yenu maalumu na muziki wenu wenye rangi tofauti na ni special.siyo kila bendi lazima ipige kama Werrason au Koffi nk.Nadhani ni vizuri wanamuziki wengine wenzetu hasa generation ya sasa wajifunze kwenu,pia wajue kuwa wanamuziki kukaa pamoja na kuwa na mshikamano
as a group ndiyo siri ya mafanikio,mmefanya vizuri sana kuwa na hii blog yenu,hata sisi wadau tuliopo ugaibuni tunapata matukio yenu yoote.Hongera sana na mkaze buti bila kuchoka.
Abbu Omar,Prof.Jnr(mwanamuziki)Tokyo,Japan.

Bila jina alisema ...

Ushauri, Kilimanjaro band ni bendi kubwa hivyo ongezeni mwanga wa taa jukwaani ili clips za video vitoke kwa ubora wa juu zaidi kama ilivyo Bendi bora na stadi ya Kilimanjaro band.

Maana Kilimanjaro Band ndiyo kioo cha muziki wa dansi na ndiyo tumewakabidhi kupeperusha jina la muziki wa Tanzania duniani. Maana ukibandika ktk youtube basi uliwengu unaona kazi toka Tanzania hivyo viwango vya video muhimu hasahasa mwanga wa kutosha jukwaani.

Mwisho hongereni kwa kazi nzuri ya kuenzi nyimbo zote zilizokuwa maarufu toka enzi na enzi iwe za Kilimanjaro band au bendi zingine za Tanzania.

Mdau
Honolulu
Visiwani Bahari ya Pasifiki.

Bila jina alisema ...

Ni kweli mdau wa Pasifiki, mimi naweza sema Kilimanjaro ni bendi bora ya Afrika Mashariki.

Ili kuweza kushikilia tunzo hiyo ya ubora basi na video vyenu ziwe na mwanga wa kutosha kuonyesha wanabendi wakifanya vitu vyao jukwaani.

Mfano nimeangalia video ya jamaa mmoja wa Kenya ktk youtube : Musa Juma- Saida VCD, kwa kweli ingawa hawezi kuifikia Kilimanjaro kwa viwango vya uana-muziki lakini shooting ya video yake ktk ukumbi wa Carnivore jijini Nairobi ni wa ubora wa hali ya juu kwa mwanga ktk jukwaa na umahiri wa mpigaji video, yaani hahamishi focus toka kwa 'image/target' moja kwenda nyingine kwa kasi ya kuharibu upigaji video n.k

Njenje mtikia maanani ubora wa video shooting zenu na mwanga wa kumulikia bendi jukwani mtakuwa mmemaliza mchezo na kutokuwa na mpinzani kimataifa, kikanda au Tanzania.

Mdau
jijini Mexico City.

Kilimanjaro band wakamilisha nyimbo mbili, kuwa hewani katika muda mfupi ujao

KILIMANJARO BAND  wananjenje jana walikamilisha kurekodi nyimbo zao mbili ambazo zitakuwa hewani katika wiki chache zijazo. Hii ni mara ya...