Monday 30 May 2011
Thursday 26 May 2011
Wednesday 25 May 2011
Njenje wapata ugeni wa K Mondo Sound
Mara kwa mara wanamuziki mbalimbali hutembelea maonyesho ya Kilimanjaro band, week-end hii wageni walikuwa bendi nzima ya K Mondo Sound wazee wa Kibajaj, ambao huwa na onyesho lao kila Ijumaa katika ukumbi wa Triz Motel Mbezi, walileta raha katika ukumbi wa Salender Bridge chini ya uongozi wa Mangustino
Monday 23 May 2011
Arusha to Dar es Salaam kupitia Kipingu Mgahawa
Baada ya Kilimanjaro Band kutumbuiza katika sherehe ya mkutano wa muungano wa Masecretary TAPSEA siku ya Ijumaa 20 May 2011, bendi ililazimika kuondoka alfajiri ya Jumamosi kuwahi onyesho la kawaida Salender Bridge Club. Safari ilienda salama mpaka tulipokaribia Korogwe ambapo barabara imeharibika kwa kuwa na mashimo mengi. Wakati wa kukwepa sehemu fulani yenye mashimo ya namna hiyo bus moja lililokuwa nyuma yetu likija spidi kali sana lilitaka kuigonga gari yetu kwa nyuma na ikalazimika dereva wetu Waziri Ally ‘Kissinger’, ajitahidi kulikwepa kwa kulazimika kuingia katika mashimo hayo gari letu lilipata pacha mbili kwa mpigo katika matairi ya upande wa kushoto. Babu Njenje aliondoka na gari lililokuwa limebeba vyombo vyetu na kwenda Korogwe mjini kutengeneza tairi hizo. Katika sehemu hiyo tulikuta mgahawa, KIPINGU MGAHAWA’ (hatuna uhakika kama ni mradi wa mwalimu Kipingu), ambao ulikuwa na chapatti safi sana, mama mmoja alikuwa akitengeneza chapatti fresh na tulizipata kwa chai ya rangi taamu. Tuliendelea na safari na kufika Dar salama. |
Chai chapati Keppy na Nyota |
Chai ya rangi |
Abuu na Nyota |
Pancha tairi mbili |
Mkutano , tunafanya nini |
Sunday 22 May 2011
NJenje Arusha
Ijumaa 20 May wanachama wa TAPSEA walipata nafasi ya kupata burudani toka kwa Kilimanjaro Band, katika ukumbi wa AICC Arusha. Mduara ulipigwa na nyonga zikazungushwa. Tena kulikuwa na kila design ya nyonga hapa.
Kibonde alikuweko |
Moddy, Abou, Babu Njenje wakisubiri |
Duara linazunguka na nyonga kwa sana |
Wenyewe wanaaiita Ekutiiiii |
Nyota |
Waziri na nyota |
Nyota akutana aliyefanana nae |
Wednesday 18 May 2011
Njenje kuwa Arusha Ijumaa 20 May, Private Function
Bendi yenu ya Kilimanjaro Band itakuwa Arusha Ijumaa 20 May 2011, kwa show ya siku moja katika 'private function '. Jumamosi jukwaani Salender Bridge as usual duara litazunguka, nyonga zitanyongwa. Kuna uwezekano mkubwa sana mpenzi maarufu wa Kilimanjaro Band Carl akatoa show kali ya nyonga......................
Sunday 15 May 2011
Jumamosi Njenje raha tele kukosa ni kosa
Kitime wa Man U, Waziri wa Njenje, Babu Njenje |
Mgongo huu ni wa Musa Masharubu |
Khaleed na filimbi!!!!!!!! |
Keppy Kiombile on Bass, Kanku Kelly the master trumpetist |
Mjomba Mgaikivembo, akiwa na Palmena Mahalu katika keyboards |
Raha ndani ya roho |
Modddyyyyyyy |
Lily na rafiki |
Mzee wa Arsenal na mwandani |
Bi Kinyau and Babu Kinyau mmeona nini? |
Kidole hichooooooo |
Saturday 14 May 2011
Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo kukutana wasanii
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dr. Emmanuel Nchimbi (Mb), atakutana na wasanii katika ukumbi wa BASATA kuanzia tarehe 17 Mei na tarehe 18 Mei, 2011. Waziri ataongea na wasanii kwa utaratibu ufuatao:-
17/05/2011 (Jumanne) Saa 4:00 asubuhi
Wasanii Wote wa Sanaa za Muziki
18/05/2011 (Jumatano) Saa 4:00 asubuhi
Wasanii Wote wa Sanaa za Ufundi,Filamu na Maonyesho
Izingatiwe kwamba Waziri ataongea na wasanii wa muziki wa aina zote wakiwemo wa Kizazi kipya,Bendi,Disco, Asili,Taarab na kadhalika katika siku ya kwanza.Katika siku ya pili yaani Tarehe 18/05/2011 ataongea na wasanii wa Sanaa za Filamu,Maonyesho na Ufundi pekee. Wasanii Wote mnaombwa kujitokeza kwa wingi.
Lengo kuu la mikutano hii kati ya Waziri na Wasanii ni kuongelea maendeleo ya fani za sanaa.
Subscribe to:
Posts (Atom)