ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

Jumatatu, 23 Mei 2011

Arusha to Dar es Salaam kupitia Kipingu Mgahawa


Baada ya Kilimanjaro Band kutumbuiza katika sherehe ya mkutano wa muungano wa Masecretary TAPSEA siku ya Ijumaa 20 May 2011, bendi ililazimika kuondoka alfajiri ya Jumamosi kuwahi onyesho la kawaida Salender Bridge Club. Safari ilienda salama mpaka tulipokaribia Korogwe ambapo barabara imeharibika kwa kuwa na mashimo mengi. Wakati wa kukwepa sehemu fulani yenye mashimo ya namna hiyo bus moja lililokuwa nyuma yetu likija spidi kali sana lilitaka kuigonga gari yetu kwa nyuma na ikalazimika dereva wetu Waziri Ally ‘Kissinger’, ajitahidi kulikwepa kwa kulazimika kuingia katika mashimo hayo gari letu lilipata pacha mbili kwa mpigo katika matairi ya upande wa kushoto. Babu Njenje aliondoka na gari lililokuwa limebeba vyombo vyetu na kwenda Korogwe mjini kutengeneza tairi hizo. Katika sehemu hiyo tulikuta mgahawa, KIPINGU MGAHAWA’ (hatuna uhakika kama ni mradi wa mwalimu Kipingu), ambao ulikuwa na chapatti safi sana, mama mmoja alikuwa akitengeneza chapatti fresh na tulizipata kwa chai ya rangi taamu. Tuliendelea na safari na kufika Dar salama.
 


Chai chapati Keppy na Nyota

Chai ya rangiAbuu na Nyota

Pancha tairi mbili

Mkutano , tunafanya nini

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

Bima ya vyombo vyenu vya muziki na nyie wenyewe mshakata? Maana sije ikawa kama mambo ya Afrosa vyombo vyao kuharibika ktk ajali ya gari na kuwa mwisho wa Bendi ya Afro 70.

Mpenzi wa Njeje.

Bila jina alisema ...

Dada Nyota na bw.Keppy,hiyo chai chapati katika Kipingu mgahawa inatutamanisha huku tuliko,nadhani ingekuwa vizuri kama mngetutumia hata kwa DHL ili nasi tupate uhondo huo,tunakosa mengi mazuri ya huko nyumbani hasa vyakula vyetu vya asili ya ki afrika,hongera kwa juhudi zenu na tupo karibu nanyi pia tunafuatilia kila hatua ya maendeleo mnayoipiga,pia nyonga za hali ya juu tunaziona zinavyoendelea huko "Mjini"Salaam kwa wana Njenje wote.We wish you all the best,
Abbu Omar,Prof.Jnr(Mwanamuziki)Tokyo,Japan.

Bila jina alisema ...

Naona mkuu Kitime ameshikilia "kikombe"nina uhakika kuwa hiki siyo kikombe cha babu,hapa ni mgahawa wa Kipingu,Watu wanaweza kushangaa maana enzi hii ni enzi ya vikombe na inafaa kuwaelewesha wapenzi wa Njenje kuwa kikombe hiki siyo cha babu wa Loliondo.Kila la kheri wana Njenje.
Abbu Omar,Prof.Jnr(Mwanamuziki)Tokyo,Japan.

Kilimanjaro band wakamilisha nyimbo mbili, kuwa hewani katika muda mfupi ujao

KILIMANJARO BAND  wananjenje jana walikamilisha kurekodi nyimbo zao mbili ambazo zitakuwa hewani katika wiki chache zijazo. Hii ni mara ya...