Sunday 4 December 2011

Buriani Mzee David Wakati, bila wewe tungekuwa wapi?

Kilimanjaro Band tunaungana na wote katika maombolezo ya kifo cha Mzee David Wakati. Mzee huyu akiwa Mkurugenzi wa RTD ndiye aliyekuwa wa kwanza kuanza kuirusha hewani   album ya kwanza ya Kilimanjaro band. Album hiyo Katakata ambayo ilirekodiwa mwaka 1989 London  ndiyo iliyokuwa na wimbo Njenje, wimbo ambayo hadi leo ndio umekuwa ndio nembo ya Bendi hii. Akiwa mkurugenzi wa radio alikuwa na kipindi chake maalumu ambapo kupitia kipindi hicho alipiga sana nyimbo toka album hii.
Mungu amlaze pema peponi Mzee wetu David Wakati  
Amen

No comments:

Post a Comment

ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA