Sunday 26 June 2011

Juma Omary, Babu Njenje, Mohamed Mrisho

Pamoja na Mduara kuzunguka jana ilikuwa siku ya ya Maonyesho ya Khanga za zamani. Wananjenje pia waliamua kutinga katika mashati ya Khanga yaliyotengenezwa na Asia Idarus ambaye alikuwa mtayarishaji wa onyesho la mavazi ya ya Khanga. KWA KWELI PALINOGA

Juma Omary, Waziri Ally, Babu Njenje, Mohamed Mrisho,

John Kitime, Juma Omary, Babu Njenje, Mohamed Mrisho Abou Mwinchumu


Tuesday 14 June 2011

HAPPY BIRTHDAY PIA BI SHAKILA NA LADY JD


Wanamuziki wengine mahiri wanasherehekea birthday yao leo nao ni Judith Wambura Lady JD, na Bi Shakila. Bi Shakila ana uhusiano wa karibu sana na Babu Njenje, walizaliwa siku moja na walizaliwa mtaa mmoja huko Tanga, mama yake Bi Shakila alipata matatizo ya  kunyonyesha hivyo Bi Shakila alianza maisha kwa kunyonya ziwa moja na Babu Njenje kwa kipindi kilekile ambacho nae Babu Njenje alikuwa ananyonya

Happy Birthday Babu Njenje

Leo tarehe 15 June, ni birthday ya Mabrouk Khamis maarufu Babu Njenje, mwanamuziki huyu wa siku nyingi aliyeanza kwa kupiga drums amefikia umaarufu wa kuimbia na kujulikana sana katika nyimbo zake za mduara kama vile Kinyaunyau, Kachiri, na baada ya recording ya album mpya ya njenje kuna nyimbo kama Kisebusebu, na Nyoka ambazo zitakuwa kumbukumbu za sauti yake daima...Happy Birthday Babu Njenje, Baba Lulu



Bado tupotupo kwanza

Tulikuwa vijana muda umepita sasa, tunamshukuru Mungu bado tupo pamoja tukifurahia maisha na kufurahisha na kuleta faraja kwa mamia ya watu Aksante Mungu kwa vipaji ulivyotupa



Monday 13 June 2011

Duh na wanaume nao kumbe wamo kwa nyongaaaaa

Bi Nyota wiki hii aliwasihi wanaume nao kuja onyesha nyonga mambo yalikuwa mambo hebu twende mjini tukaone

Saturday 11 June 2011

Sherehe ya harusi ya Machapati

 
Mpenzi maarufu wa Kilimanjaro Band Juma Machapati kaoa wiki hii na akaona ni bora sehemu yasherehe aihamishie katika onyesho la Njenje. Kulikuwa na patashika nguo kuchanika , Machapati na Mkewe pichani walianza sherehe kwa wimbo uitwo Kisebusebu na Kirohopapo, Champagne zilifunguliwa, Keki zilikatwa, nyonga zilikatwa, zawadi kemkem zilimiminika. Wanamuziki wa Kilimanjaro Band wanawatakia maharusi ndoa njema ya raha itakayodumu






Sunday 5 June 2011

Nyimbo mpya yapokelewa kwa shangwe

Waziri Ally alitangaza kuwa kuna nyimbo mpya ambayo wapenzi wangeonjeshwa kwa hiyo watayarishe nyonga, kwa kweli matokeo yake ni ya ajabu sana. Wakati wimbo ukiendelea wapenzi waliucheza, wengine wakavamia jukwaa, na kumtuza fedha nyingi Nyota ambaye alikuwa akiimba wimbo huo. Ni mara ya kwanza kuona watu wakipanda jukwaani na kuanza kukumbatia wanamuziki kwa kupiga nyimbo mpya. Aksante Mungu kwa kutupatia kipaji hiki

Mambo ya Jumamosi 4, pale Salender Bridge


Khalid akimsaidia Abou katika Conga

Oyaa we Mzee mawani yatadondoka hayoooo

Mgeni wa leo George Gama katika bass

Duhhh mi thithemi lakini kuwa mwanamuziki raha



Oyaa Wadhiri unafurahia nini?

"Jamani  Waziri chukua huyu Msimbazi jamani"

Saturday 4 June 2011

Mazoezini kwa ajili ya album mpya

 
Kuna ule wakati mnatengeneza wimbo halafu mnakuwa na uhakika watu wataupokea vizuri, mnaanza kufurahi kabala ya kuutoa hadharani. Huu wimbo atakaoimba Nyota ni wa aina hiyo....Mbite mbite ........



ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA