Saturday 25 February 2012

Warithi wa Njenje jukwaani

Kilimanjaro Band inaamini kuwa ni muhimu kurithisha mzigo huu wa muziki kwa vijana ili nao waendeleze kazi hii. Mara kwa mara vijana wenye vipaji wamekuwa wanakuja na kujiunga na bendi jukwaani na kuonyesha vipaji vyao katika kuimba na hata kupiga vyombo. Jana alipita binti Salma Chuchu ambaye alifuatana na baba yake na mama yake ambao ni wapenzi wa kubwa wa bendi ya Njenje na Salma alipanda jukwaani na kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika kupiga na kuimba. Kumbukeni hili jina SALCHU mtalisikia sana katika ulimwengu wa muziki. aboubakary Mzuri ambaye alianza kusikika na kujulikana baada ya kushiriki vizuri katika BSS, nae ni kati ya vijana ambayo hupanda jukwaa la Njenje na kuonyesha vipaji vyao. Bendi imekuwa ikimpigia muziki katika wimbo ambao kautunga mwenyewe PESA NIONEE HURUMA.
SalChu




Unamkumbuka Aboubakary Mzuri

Babu katikati ya wajukuu

babu Njenje na Abou Mzuri

Salma Chuchu

Saturday 18 February 2012

Baada ya safari ya Arusha, Njenje uwanja wa nyumbani

Pamoja na kuwa na onyesho katika viwanja vya  Mount Meru Hotel Arusha siku ya Ijumaa usiku, wanamuziki wa Kilimanjaro Band waliwahi usafiri wa Kilimanjaro Express alfajiri ya Jumamosi ili kuwahi onyesho lao la kawaida pale Salender Bridge. Onyesho lilifana kwa kuwa na watu wengi sana. Pamoja na wote pia mwanamuziki Anania Ngoliga alipanda katika jukwaa la Njenje mara kadhaa na kutoa burudani kali


,

Friday 17 February 2012

Njenje Wakiwa Arusha kwenye sherehe baada ya mkutano wa Tanzania Law Society

Kama ambavyo imekuwa ikitokea kwa miaka kadhaa mfululizo Kilimanjaro Band tena ilipewa heshima ya kutumbuiza katika sherehe ya wanachama wa Tanzania Law Society. Safari hii mkutano ulikuwa Arusha, na jioni tulivu iliyokuwa na 'dinner' na Dance ilikuwa katika viwanja vya Mount Meru Hotel Picha za matukio hizo hapo.

Chini ya uangalizi makini wa Louis kifanga Babu Njenje anaandaa nyaya

Matayarisho ya steji

Moddy akitayarisha gitaa




Nyama choma


Life time award




Kata kata










ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA