Sunday 30 March 2014

WAIMBAJI VIJANA WA NJENJE


Kutana na waimbaji vijana wa Njenje ambao ni wazi wanakipaji kikubwa cha uimbaji na kuburudisha jukwaani. Kila Jumamosi utawakuta wakifanya mambo yao Njenje
Seleman


Aboubakary Mzuri



BAADA YA MVUA KUBWA WIKI HII MDUARA WA NJENJE ULIZUNGUKA SALAMA MIPICHA YA WANAMUZIKI


















Friday 28 March 2014

MSIBA MKUBWA, PUMZIKA KWA AMANI AGNES KABALO MNGUTO

The Kilimanjaro Band imepata msiba mzito kwa kifo cha Agnes Mnguto aliyekuwa mke wa Meneja wa muda mrefu wa Kilimanjaro Band, Steven Mnguto. Agnes mwenyewe alikuwa mpenzi mkubwa wa kilimanjaro Band. Mungu amlaze pema peponi

Tuesday 25 March 2014

NJENJENI JUMAMOSI HII

KAMA kawaida siku ya Jumamosi kuanzia mida ya saa nne na nusu usiku The Kilimanjaro Band huanza maonyesho yake pale Salander Bridge Club , duara huanza kuzungushwa na muziki kutoka kila pande ya dunia hupigwa, nyimbo za Kiarabu, Kihindi, Kispanish, kihehe, Kinyakyusa na makabila mengine husikika Jumamosi hii pia mambo yaliwaka kama kawa. Wanamuziki wa Njenje kazini




Sunday 9 March 2014

BABU NJENJE APANDA JUKWAANI KWA MARA YA KWANZA TOKA 9 DESEMBA 2013


BABU NJENJE,  kwa jina halisi Mabrouk Khamis, jana Jumamosi tarehe 8 March 2014 alipanda tena jukwaani na kushirikiana na bendi yake Kilimanjaro Band aliimba nyimbo kadhaa ambazo zinapendwa na wapenzi wa bendi hiyo. Babu Njenje alipata stroke tarehe 9 December 2013 wakati akijitayarisha kwenda kwenye onyesho la bendi hiyo lililokuwa lifanyike katika ukumbi wa Escape One kusherehekea siku ya Uhuru. Katika kupata stroke hiyo aliathirika mguu na mkono wa kushoto. Taratibu katika kipindi hiki amekuwa anapewa matibabu na hatimae jana akafika jukwaani na kuimba nyimbo zake. Pamoja na kuwa bado anaendelea na matibabu kwa bado hawezi kusimama na anahitaji wheelchair kusafiri, lakini Mungu ni wa kushukuriwa hadi hapa alipofika. Kwa taarifa yake mwenyewe aliwashukuru wapenzi wa Njenje na kumtaja haswa BI Salma Mtambo kwa kumwezesha kufikia hali hiyo ya afya.

ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA