Friday 30 May 2014
Saturday 10 May 2014
NJENJE WAAnZA MATAYARISHO YA ALBUM MPYA
Kilimanjaro Band imeanza mazoezi makali ya kutengeneza album mbili katika mwaka huu. Album hizi, moja ikiwa THE BEST OF KILIMANJARO BAND itakusanya nyimbo zote zilizopendwa zaidi katika mkusanyiko wa album zote za Kilimanjaro Band zilizopo. Pia kutakuwa na album yenye nyimbo mpya ambamo kutakuweko na nyimbo kama Nyoka na Kisebusebu ambazo zinapigwa tayari na bendi na zimetokea kupendwa sana katika maonyesho ya bendi. Nyimbo mbili za zamani sana zilizofanywa upya mazoezi zitaanza kupigwa katika maonyesho ya Kilimanjaro band kuanza wiki hii. Ukiwemo wimbo kutoka album ya kwanza ya bendi hii KATAKATA. Mazoezi ya bendi hii yanafanyika kila siku ya wiki kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nane mchana. Hii ni kuweza kufanya kazi wakati akili zikiwa bado fresh ili kupata kitu bora kwa wapenzi wa muziki wa Njenje. Miaka miwiwli iliyopita Njenje walijipanga kutoa album mpya lakini ushauri wa kibiashara ulitolewa kuishauri bendi isubiri kwanza kabla ya kutoa album nyingine. Bendi imeshatimiza miaka 40 ikiwa jukwaani
Subscribe to:
Posts (Atom)