Saturday 23 August 2014

BABU NJENJE ATEMBELEWA NA WANAMUZIKI WALIOSHIRIKI KWENYE FIESTA TANGA


Babu Njenje ambaye alipata stroke tarehe 9 December 2013, na ambaye kwa muda huu yuko Tanga kwa matibabu na mapumziko alipata ugeni mkubwa wa wanamuziki walioshiriki katika Tamasha la Fiesta kule Tanga. Hali ya Babu Njenje ambayo inaimarika kila siku kwa vyovyote iliongezea mengi na upendo uliofanywa na wanamuziki hawa.
Wakati huo huo mwanamuziki mwingine wa Kilimanjaro Band, Abou Mwinchumu amefanyiwa opereshen ya tonsils wiki hii na hataweza kushiriki katika maonyesho ya bendi kwa muda mpaka atakapopata nafuu. Bendi inaendelea na maonyesho na kutakuweko na mwimbaji mpya kijana ambaye ameonyesha uwezo mkubwa wa kuimba atakae chukua mzigo huo ulioachwa na Babu Njenje na Abou kwa picha za wasanii wakiwa na Babu Njenje ingia hapa

No comments:

Post a Comment

ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA