Sunday 23 February 2014

NJENJENI MAMBO MATAMUUU







NJENJENI JUMAMOSI 22 FEBRUARI 2014

Pamoja na kukumbwa na dharuba ya kuugua ghafla kwa mwimbaji mkuu wa bendi hii Mabrouk Khamis Babu Njenje, bendi imeendelea kufanya maonyesho kila Jumamosi katika ukumbi wa Salender Bridge kuanzaia saa nne na nusu hadi alfajiri. Babu Njenje alipata stroke alasiri ya tarehe 9 Dec 2013, wakati akijitayarisha kwa ajili ya onyesho la bendi kwenye ukumbi wa Escape One kusherehekea siku ya Uhuru. Kuanzaia hapo muda mwingi amekuwa kitandani, awali alikuwa hawezi hata kunyanyua mguu na mkono wake wa kushoto, lakini kwa uwezo wa Mungu matibabu anayayapata yamemwezesha sasa kuweza kuanza kutembea na kunyanyua mkono wa kushoto. Mungu akipenda atakuwa jukwaani tena muda si mrefu.
Kijana Abou Mwinchumu ambae huwa pia ni mpiga percussion amekuwa ndie mziba pengo kwa kuweza kuimba nyimbo zote maarufu za Babu Njenje na hivyo kwa mgeni kutokutambua kuwa kuna tofauti. Hii hapa kazi ya ya Jumamosi hii.
Mohamed Moddy Mrisho

Shaaban

Abou Mwinchumu kiraka

Bibie Nyota hapa akiimba Gere, chezea Nyota wewe?

ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA