Sunday 20 April 2014

Unamkumbuka Dullah mwanamuziki aliyepitia Msondo kisha Kilimanjaro Band na hatimae Tatunane?


DULLAH ni mmoja wa wanamuziki wa awali wa Kilimanjaro Band, aliacha bendi na kujiunga na kundi la Watafiti ambalo hatimae likawa TatuNane, kwa sasa Dullah yuko Denmark akiendelea na muziki hebu tumuone hapa akiwa jukwaani katika show moja ya Copenhagen Festival, ambapo mpenzi mmoja wa muziki alipanda na kuanza kumwaga nyonga za nguvu. Waliomo katika bendi hii Dulla Mnanga band ni: Dulla Mnanga: Vocal, guitar, percussions, Carsten Svanberg: Keyboards. Kristian Hybel: Bass. guitar Katrine Suwalski: Sax, backing vocals, percussions. Peter Suwalski: Drums. Camilla Groth Clausen: Percussion. Ukitaka kujua zaidi kuhusu kundi hili ingia www.facebook.com/dullamnangaband. Kwa kukodi: PeterJ@Suwalski.Com.

Sunday 13 April 2014

MZEE MUHIDIN MAALIM GURUMO AFARIKI DUNIA


Mwanamuziki muimbaji wa miaka mingi Mzee Muhidi Maalim Gurumo hatunae tena. Mzee Gurumo amefariki alasiri hii katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Mungu amlaze Pema Peponi..AMIN

Sunday 6 April 2014

KAMA KAWA JUMAMOSI HII KULIKUCHA

Pamoja na wengi walioingia Njenje Jumamosi hii pia alikuweko Senetor mmoja kutoka Marikani, dancer kutoka New York akiwa na mumewe ambaye ni mwanasheria wa mambo ya sheria za kazi za burudani, Ben Kinyaiya pia alionekana ndani ya nyuma Miss Kiswahili Rehema Fabian nae alikuweko. Na wapenzi wa daima akina Machapata na kundi lake, Kossovo na familia yake, na wengiiiii waliduarika kama kazi. Usikose Jumamosi ijayoooo
MODDY

WAZIRI

MWINCHUMU

KITIME NA KEPI

YUSUFFFFF






NYOTA




DOH KITIME ANAMWAGA MIUNO

KUNANI PALEEE?


ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA