Friday 30 May 2014

REST IN PEACE GEORGE TYSON

WANAMUZIKI wote wa Kilimanjaro Band tunachukua nafasi hii kutoa pole kwa familia ndugu na marafiki wa Director na rafiki yetu George Tyson. Mungu awape uvumilivu na amlaze Pema George Tyson Amen

Saturday 10 May 2014

NJENJE WAAnZA MATAYARISHO YA ALBUM MPYA

Kilimanjaro Band imeanza mazoezi makali ya kutengeneza album mbili katika mwaka huu. Album hizi, moja ikiwa THE BEST OF KILIMANJARO BAND  itakusanya nyimbo zote zilizopendwa zaidi katika mkusanyiko wa album zote za Kilimanjaro Band zilizopo. Pia kutakuwa na album yenye nyimbo mpya ambamo kutakuweko na nyimbo kama Nyoka na Kisebusebu ambazo zinapigwa tayari na bendi na zimetokea kupendwa sana katika maonyesho ya bendi. Nyimbo mbili za zamani sana zilizofanywa upya mazoezi zitaanza kupigwa katika maonyesho ya Kilimanjaro band kuanza wiki hii. Ukiwemo wimbo kutoka album ya kwanza ya bendi hii  KATAKATA. Mazoezi ya bendi hii yanafanyika kila siku ya wiki kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nane mchana. Hii ni kuweza kufanya kazi wakati akili zikiwa bado fresh ili kupata kitu bora kwa wapenzi wa muziki wa Njenje. Miaka miwiwli iliyopita Njenje walijipanga kutoa album mpya lakini ushauri wa kibiashara ulitolewa kuishauri bendi isubiri kwanza kabla ya kutoa album nyingine. Bendi imeshatimiza miaka 40 ikiwa jukwaani





ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA