Saturday 23 August 2014

BABU NJENJE ATEMBELEWA NA WANAMUZIKI WALIOSHIRIKI KWENYE FIESTA TANGA


Babu Njenje ambaye alipata stroke tarehe 9 December 2013, na ambaye kwa muda huu yuko Tanga kwa matibabu na mapumziko alipata ugeni mkubwa wa wanamuziki walioshiriki katika Tamasha la Fiesta kule Tanga. Hali ya Babu Njenje ambayo inaimarika kila siku kwa vyovyote iliongezea mengi na upendo uliofanywa na wanamuziki hawa.
Wakati huo huo mwanamuziki mwingine wa Kilimanjaro Band, Abou Mwinchumu amefanyiwa opereshen ya tonsils wiki hii na hataweza kushiriki katika maonyesho ya bendi kwa muda mpaka atakapopata nafuu. Bendi inaendelea na maonyesho na kutakuweko na mwimbaji mpya kijana ambaye ameonyesha uwezo mkubwa wa kuimba atakae chukua mzigo huo ulioachwa na Babu Njenje na Abou kwa picha za wasanii wakiwa na Babu Njenje ingia hapa

Thursday 7 August 2014

NJENJE YANUNUA GITAA LA AJABU

GITAA JIPYA AINA YA YAMAHA
Mohamed Mrisho akiwa na Gitaa hili la ajabu ambalo unaweza kulibomoa vipandevipande na kuwa dogo kuweza kukunja na kutembea nalo. Pia unaweza kufanya mazoezi kwa kutumia headphone bila mtu mwingine kulisikia. Gitaa hili lilianza kutumika siku ya Idd Mosi..

PICHA ZA ONYESHO LA JUMAMOSI TAREHE 2 AUGUST








KILIMANJARO BAND YAPATA KINANDA KIPYA


,

Kilimanjaro Band imenunua kinanda kipya aina ya YAMAHA MOXF8, moja ya vinanda vipya vilivyotolewa na kampuni hiyo maarufu karibuni. Kinanda hicho ambacho thamani yake ni USD 1999 kimeanza kutumika toka onyesho la Idd Mosi na kitatumika katika nyimbo mpya zinazotengezwa na bendi hii.


ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA