Friday 13 November 2015

SHAMBULIO LA RISASI KATIKA ONYESHO LA MUZIKI WATU 100 WAUWAWA

KATIKA  shambulio ambalo lilianza kwa kuteka watu waliokuwa wakisikiliza na kucheza muziki wa bendi ya Eagles of Death Metal, katika ukumbi wa Bataclan huko Paris, watu 100 wameuwawa. Shambulio hilo ambalo serikali ya huko imelitamka kuwa ni la kigaidi, lilikuwa moja ya mashambulio zaidi ya sita ambayo yalipangwa kwa pamoja, ambayo yamesababisha mpaka sasa vifo vya watu 140. Mpaka sasa wanamuziki wa bendi ya Eagles of Death Metal hawajulikani waliko au kama ni kati ya waliouwawa na magaidi. Mashambulio 7 yalifanywa katika sehemu mbalimbali katika jiji la Paris, ikiwemo ulipuaji wa bomu katika bar jirani ya uwanja wa mpira ambako kulikjuwa na mechi na kufyatulia risasi watu waliokuwa wanakula. Mpaka sasa hali ni tetet kwani bado washambuliaji wengine hawajakamatwa.

ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA