Saturday 14 May 2011

Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo kukutana wasanii




Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dr. Emmanuel Nchimbi (Mb), atakutana na wasanii katika ukumbi wa BASATA kuanzia tarehe 17 Mei na tarehe 18 Mei, 2011. Waziri ataongea na wasanii kwa utaratibu ufuatao:-

17/05/2011 (Jumanne) Saa 4:00 asubuhi
Wasanii Wote wa Sanaa za Muziki

18/05/2011 (Jumatano) Saa 4:00 asubuhi
Wasanii Wote wa Sanaa za Ufundi,Filamu na Maonyesho




Izingatiwe kwamba Waziri ataongea na wasanii wa muziki wa aina zote wakiwemo wa Kizazi kipya,Bendi,Disco, Asili,Taarab na kadhalika katika siku ya kwanza.Katika siku ya pili yaani Tarehe 18/05/2011 ataongea na wasanii wa Sanaa za Filamu,Maonyesho na Ufundi pekee. Wasanii Wote mnaombwa kujitokeza kwa wingi.
Lengo kuu la mikutano hii kati ya Waziri na Wasanii ni kuongelea maendeleo ya fani za sanaa.






No comments:

Post a Comment

ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA