ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

Jumapili, 5 Novemba 2017

KILIMANJARO BAND JUKWAANI ARUSHA IJUMAA 3 NOVEMBA 2017


MVUA ZAVUNJA ONYESHO LA JUMAMOSI LA KILIMANJARO BAND

MVUA zilizopiga siku nzima jana JUmamosi zimesababisha onyesho la kila wiki la Njenje kutokufanyika. Wananjenje ambao siku ya Ijumaa walikuwa Arusha waliweza kuwahi kufika Dar tayari kwa onyesho lao, lakini hali ya hewa haikuwa rafiki kwa onyesho.
Wapenzi wote mnakaribishwa tena Jumamosi ijayo kama kawaida

Ijumaa, 3 Novemba 2017

KILIMANJARO BAND WAKO ARUSHA KWA AJILI YA KUTOA BURUDANI KWA WAJUMBE WA MKUTANO WA TANZANIA REINSURANCE COMPANY LTD
ILIPOFIKIA BENDI SOUND CHECK
KUNDI LA NGOMA KUTOKA ARUSHA LIKIBURUDISHA HADHAARA KWA NGOMA YA KIBATI

NYOTA ABDALLAH MUIMBAJI

SHABAN MPIGA BASS  

ABOU MWINCHUMU CONGA NA KUIMBAWAZIRI ALLY KUIMBA NA KINANDA


KEPPY KIOMBILE -BASS NA SOUND ENGINEER

Jumanne, 24 Oktoba 2017

NJENJE STUDIONI TENA

Ni muda mrefu toka kilimanjaro Band haijaingia studio kurekodi nyimbo zake. Wiki mbili zilizopita kazi hii ilianza kwa bendi kuanza kurekodi nyimbo 3. Wapenzi wa Njenje karibuni mtapata kusikia tena kazi mpya.

Alhamisi, 24 Agosti 2017

ILIKOTOKEA KILIMANJARO BAND


Santuri ya kwanza ya Kilimanjaro Band

Kwenye miaka ya sabini kundi la vijana mjini Tanga walianzisha bendi wakajiita The Love Bugs, kundi hili lilikuwa  mchanganyiko wa Magoa na Waafrika, hususan likawa  linapiga nyimbo za wanamuziki wengine hasa kutoka Ulaya na Marekani, baada ya muda vijana hawa wakabadili jina na kujiita the Revolutions na kuhamia Dar Es Salaam. ambapo waliweza kujiweka katika nafasi ya juu kwa bendi zilizokuwa zikipiga mahotelini kwa wakati ule. The Revolutions waliweza kupiga katika hoteli kubwa mbalimbali katika miji ya Arusha and Dar es Salaam. Mwaka  1989 bendi ilienda London kwa mara ya kwanza na huko ikabadilisha jina na kujiita Kilimanjaro Band,wakati ikiwa huko bendi ilitoa album yake ya kwanza‘Kata kata”. Album yenye nyimbo mchanganyiko wa mahadhi na pia lugha. Kata kata wenyewe ulikuwa ni wimbo wa Kiingereza. Katika album hiyo pia ndiyo ulirekodiwa wimbo Njenje ambao umekuwa ukipendwa hadi leo na pia kusababisha bendi hii kuitwa Wananjenje

REST IN PEACE BABU FRANCIS


BABU FRANCIS AZIKWA KOROGWE MUNGU AILAZE ROHO YAKE PEMA PEPONI. KILIMANJARO BAND HAITAKUSAHAU

Jumatano, 23 Agosti 2017

BABU FRANCIS WA NJENJE KUZIKWA KESHO KOROGWE

Baada ya Misa iliyofanyika katika kanisa la St Nicholaus lililopo Mtaa wa Arusha  Ilala  Dar es Salaam, mwili wa aliyekuwa mweka hazina wa Kilimanjaro Band, Francis Mnguto hatimae ulisafirishwa kwenda kuzikwa Korogwe. Maamuzi ya kuzikwa Korogwe yalifikiwa na ndugu na kubadilisha maamuzi ya awali ya kumzika Francis jijini Dar es Salaam.  Francis atazikwa kesho Alhamisi.
Mungu Amlaze Pema Francis

Jumapili, 20 Agosti 2017

MSIBA MKUBWA NJENJE

MWEKA HAZINA  wa miaka mingi wa Kilimanjaro Band, ambaye alijulikana kwa wapenzi wengi kutokana na kuwa mkata tiketi wa bendi wa miaka mingi sana, Francis Mnguto, maarufu kwa jina la Babu Francis amefariki leo alfajiri nyumbani kwake Ilala Flats Dar es Salaam. Kwa miezi kadhaa Babu Francis amekuwa akisumbuliwa na tatizo la figo. Taarifa kutoka kwa familia ni kuwa mazishi yatakuwa Dar es Salaam Jumatano 23 Agosti. Msiba upo nyumbani kwake Ilala Flats Dar es Salaam.