![]() |
KUMBURU |
Baada ya kifo ya Waziri Ally, kiongozi na mpiga kinanda wa Kilimanjaro
Band, bendi ilipata pigo kubwa ambalo limechukua muda mrefu kupata ahueni.
Ili kuendeleza bendi hii kongwe iliyoanza mwanzoni mwa miaka ya 70 kule Tanga,
wanamuziki wapya watatu wamejiunga na kuanza mazoezi makali na bendi hii.
Kwanza kabisa kuna mkongwe Geophrey
Kumburu, huyu ni mpiga kinanda wa miaka mingi ambaye kati ya bendi alizopitia
ni Kilimanjaro Connection, MK Group, Vijana Jazz band,Wahenga band, JFK Band na
kwa miaka mingi alikuwa akifanya kazi peke yake ikiwemo kuendesha na studio ya kurekodi muziki. Na kufundisha
muziki. Geophrey pia ni muimbaji na ndie amechukua jukumu la kupiga kinanda
katika bendi hii kongwe. Pia kuna vijana wadogo wawili ambao ni waimbaji,
Martha na Feisal ambao ni wazi uwezo wao uko juu na utaleta nmchango mkubwa
katika Kilimanjaro band.
No comments:
Post a Comment