Baada ya shughuli za uchaguzi kwisha mduara umezunguka kama kawaida. Ukumbi unaboreshwa kwa kuezekwa na makuti na hivyo kupendeza na kuwezesha watu kukaa na kustarehehata kama mvua itanyesha. Jana ilikuwa Birthday ya Waziri Ally, kijana mdogo aliyemaliza 'seven' juzijuzi, Angel Mganga nae katimiza mwaka mwingine , Rachel alihakikisha bendi inalitambua hilo na kuhakikisha anaimbiwa wimbo wa birthday ukifuatiwa na mduara wa nyimbo mpya ya Nyoka. Zee la Nyeti na yule mtangazaji wa Times FM Alice walionyesha umahiri wao wa kukaa kwenye viti kwa muda mrefu bila kuumia. Mkali moja toka Temeke aliomba kurushwa watu wajue anakaa Temeke mtaa wa Sabasaba, Mashauzi alikuwepo, Musa Masharubu alikuweko. Joe Shumbusho alikuwa ndani ya nyumba baada ya kupotelea Marikani tangu miaka ya tisini, Eva Mbwana nae karudi Bongo baada ya kuweko UK kwa miaka nenda rudi , na alicheza nyimbo zoooooooooooote, chini ya ushauri wa Claire.
Eva in the middle of her brothers
Nina dume langu dume kila siku makelele |
Kituo cha kazi shusha...wanasikika Times FM |
Musa Masharubu |
Man U |
Man United teh teh teh |
Nyota na Abou the percusionist |
Zee la Nyeti mduarani |
nauza vioo Kariakoo |
Miuno |
Miuno zaidi |
Kosovo and wife |
Lambwalambwa lambwatika |
Watasema mchanaee usiku watalala |
Kweli pombe si chai.
ReplyDelete