Saturday, 25 February 2012

Warithi wa Njenje jukwaani

Kilimanjaro Band inaamini kuwa ni muhimu kurithisha mzigo huu wa muziki kwa vijana ili nao waendeleze kazi hii. Mara kwa mara vijana wenye vipaji wamekuwa wanakuja na kujiunga na bendi jukwaani na kuonyesha vipaji vyao katika kuimba na hata kupiga vyombo. Jana alipita binti Salma Chuchu ambaye alifuatana na baba yake na mama yake ambao ni wapenzi wa kubwa wa bendi ya Njenje na Salma alipanda jukwaani na kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika kupiga na kuimba. Kumbukeni hili jina SALCHU mtalisikia sana katika ulimwengu wa muziki. aboubakary Mzuri ambaye alianza kusikika na kujulikana baada ya kushiriki vizuri katika BSS, nae ni kati ya vijana ambayo hupanda jukwaa la Njenje na kuonyesha vipaji vyao. Bendi imekuwa ikimpigia muziki katika wimbo ambao kautunga mwenyewe PESA NIONEE HURUMA.
SalChu




Unamkumbuka Aboubakary Mzuri

Babu katikati ya wajukuu

babu Njenje na Abou Mzuri

Salma Chuchu

No comments:

Post a Comment

ON STAGE

ON STAGE
ON STAGE

TUNAANZA MWAKA NA NGUVU MPYA