Onyesho la muziki la Kilimanjaro Band jana lililazimika kuongeza muda kutokana na wapenzi wa muziki kugoma kutoka ukumbini licha ya TANESCO kukata umeme kwa zaidi ya saa nzima kuanzia muda wa saa 8 usiku, na hivyo bendi kulazimika kupiga mpaka karibu kunakucha. Kama kawaida ya maonyesho ya bendi ya Kilimanjaro, wapenzi wake huanza hasa kuingia ukumbini baada ya saa tano usiku, na kufikia saa saba ukumbi ndo unakuwa umefurika na raha za miduara na muziki wa aina nyingine kujaa angani, watu wastaarab wakiendelea na raha zao. Kwa usiku wa jana na kama ambavyo imekuwa kawaida siku hizi kundi la East African Melody nalo limekuwa likipita na kufanya show zao wakati huohuo, hivyo kuwapa wapenzi raha mara mbili. Siku ya jana iliongezeka kwa Njenje kutembelewa na wanamuziki wengine akiweko Anania Ngoliga aliyependa jukwaani na kuporomosha kibao maaruf cha Tabu Ley ‘Maze’, na mwanamuziki huyu asiyeona kupiga gitaa la solo na kuimba wakati huohuo. Wanamuziki kadhaa walikuja kuongezeka hasa wakati wa wimbo wa Gere ambao huimbwa na bibie mwenye sauti tamu Nyota Abdallah, wasanii kama Khadija Kimobitel na Maria Salome, mcheza show wa Twanga Pepeta walipanda jukwaani na kuonyesha umahiri wao wa kukata nyonga.
It was fun
No comments:
Post a Comment