The kilimanjaro Band of Tanzania
Tuesday, 10 January 2023
Monday, 26 December 2022
MKUTANO WA MWISHO WA MWAKA WA NJENJE FAN CLUB WAFANA
WAPENZI wa Kilimanjaro Band katika kundi lao linalojulikana kama Njenje Fan Club wakiwa na baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo, leo walikuwa na mkutano wao wa kufunga mwaka 2022. Kilimanjaro Band inatarajiwa kuanza kufanya maonyesho ya kawaida ya kila wiki mapema mwanzoni mwa 2023. Bendi imo katika matayarisho ya kusherehekea miaka 50 toka kuanzishwa kwa bendi hiyo.
![]() |
Geophrey Kumburu - mpiga keyboards Kilimanjaro Band |
Friday, 14 October 2022
Friday, 30 September 2022
Wednesday, 28 September 2022
Monday, 26 September 2022
KILIMANJARO BAND WAWASHA MOTO DODOMA, IT WAS GREAT
![]() |
Nyota Abdallah |
JUMAMOSI tarehe 24 Septemba 2022 ilikuwa siku ambayo kwa mara ya kwanza bendi ya Kilimanjaro Band ilifanya onyesho katika uwanja wa maegesho ya magari wa Capital City Mall. Muziki ulianza rasmi saa 4 usiku kwa muziki wa taratibu na ilipofika saa tano Njenje wakaanza kwa kupiga wimbo maarufu wa Njenje. Kisha kukawa na mchanganyiko wa aina mbalimbali za muziki kama ilivyo kawaida ya bendi hii. Vijana wadogo wapya ambao wamechukuliwa kuendeleza bendi hii hakika waliweza kuzikonga nyoyo za washabiki wakiokuwepo katika onyesho hilo.
![]() |
Martha, muimbaji mpya wa Kilimanjaro Band |
![]() |
Abou Mwinychumu |
![]() |
Mkongwe Mohamed 'Moddy' Mrisho |
![]() |
John kitime |
Thursday, 1 September 2022
NJENJE NDANI YA DODOMA KWA MARA YA KWANZA UNAKOSAJEEE?
The Kilimanjaro Band will be in Dodoma for the first time on 24th September 2022, how can you possibly miss the event?
Monday, 29 August 2022
WANAMUZIKI WATATU WAJIUNGA NA KILIMANJARO BAND
![]() |
KUMBURU |
Baada ya kifo ya Waziri Ally, kiongozi na mpiga kinanda wa Kilimanjaro
Band, bendi ilipata pigo kubwa ambalo limechukua muda mrefu kupata ahueni.
Ili kuendeleza bendi hii kongwe iliyoanza mwanzoni mwa miaka ya 70 kule Tanga,
wanamuziki wapya watatu wamejiunga na kuanza mazoezi makali na bendi hii.
Kwanza kabisa kuna mkongwe Geophrey
Kumburu, huyu ni mpiga kinanda wa miaka mingi ambaye kati ya bendi alizopitia
ni Kilimanjaro Connection, MK Group, Vijana Jazz band,Wahenga band, JFK Band na
kwa miaka mingi alikuwa akifanya kazi peke yake ikiwemo kuendesha na studio ya kurekodi muziki. Na kufundisha
muziki. Geophrey pia ni muimbaji na ndie amechukua jukumu la kupiga kinanda
katika bendi hii kongwe. Pia kuna vijana wadogo wawili ambao ni waimbaji,
Martha na Feisal ambao ni wazi uwezo wao uko juu na utaleta nmchango mkubwa
katika Kilimanjaro band.
Thursday, 25 August 2022
TANZIA MZEE ALLY SEIF, BABA YAKE WAZIRI ALLY AFARIKI TANGA
Tuesday, 16 August 2022
KILIMANJARO BAND NJENJE YAANZA KUJIFUA KURUDI ULINGONI
NI mwaka mmoja toka mpiga kinanda na kiongozi wa Kilimanjaro Band Waziri Ally Seif alipofariki, bendi ya Kilimanjaro, wana Njenje walikuwa kimya kwa kipindi karibu chote, sasa bendi hiyo imo katika mazoezi makali na inategemea kuanza onyesho lake la kwanza katika jiji la Dodoma kabla ya mwisho wa mwezi huu. Usikose kutembelea humu kupata taarifa za ratiba ya bendi hii.
ON STAGE

ON STAGE